Published On: Thu, Jun 14th, 2018

SERIKALI YAANZA MSAKO WA WAFANYABIASHARA WANAOLANGUA PEMBEJEO ZA KOROSHO TUNDURU

Share This
Tags

Serikali wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma imesema itaanza kufanya msako wa kuwabaini wafanyabiashara wa pembejeo za zao la Korosho wanaouza kwa bei ya juu, ili kuwalangua wakulima kinyume na bei elekezi iliyopangwa na Bodi ya Korosho Tanzania CBT ya shilingi elfu thelathini na mbili kwa mfuko mmoja wa Salfa.

Akizungumza katika uzinduzi kugawa pembejeo hizo wilayani humo, mkuu wa wilaya ya Tunduru JUMA HOMELA amesema wamebaini kuwepo kwa ulanguzi huo ambapo kuna watu  wanaonunua pembejeo katika vyama vya msingi kwa bei ya serikali na kwenda kuwauzia wakulima kwa kianzio cha shilingi elfu 60 na zaidi.

Wakulima wa zao hilo waliofika katika uzinduzi huo, wakaishukuru serikali kwa kuwahisha pembejeo hizo kwa wakati, huku wakiahidi kuongeza uzalishaji kwa kufufua mashamba yao ambayo waliyatelekeza.

Bodi ya Korosho Tanzania inaendelea na zoezi la uzinduzi wa ugawaji wa pembejeo hizo na viuatilifu vya maji katika wilaya mbalimbali zinazolima Korosho kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa zao hilo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>