Published On: Wed, Jun 13th, 2018
Sports | Post by jerome

Rwanda yapanda daraja, sasa kutangaza njia mpya itakayotumika mwaka huu

Share This
Tags

Shirikisho la mchezo wa mbio za Baiskeli nchini Rwanda FERWACY  leo mchana linatarajiwa kutangaza barabara mpya zitakazounda mzunguko mzima wa mashindano ya kimataifa kwa mwaka huu ya nchini humo, mtandao wake ukitarajiwa kuwa mpya na wa daraja la juu kwa kuwa mabadiliko haya ni kwa mujibu wa kanuni zinazoongoza mchezo huo duniani.

Mashindano haya ni awamu ya kumi tangu taifa hilo lianze kuandaa, na yanatarajiwa kuanza rasmi Agosti 5 na kumalizika Agosti 12, ikiwa ni tofauti na ratiba ya miaka iliyopita ambapo Rwanda ilikuwa inaandaa mashindano hayo mnamo mwezi Novemba.

Kwa viwango vya dunia Rwanda sasa inakuwa nchi ya pili kwa barani Afrika kupanda daraja la viwango vya ubora wa mashindano kutoka 2.2 kwenda 2.1, kwani mpaka sasa ni taifa la Gabon pekee ndio lilikuwa na kiwango hicho.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>