Published On: Sat, Jun 30th, 2018
Science | Post by jerome

Roboti Sophia yapoteza mikono yake ikiwa safarini kwenda Ethiopia

Share This
Tags

Sophia, roboti maarufu mfano wa binadamu, imewasili nchini Ethiopia bila sehemu zingine za mwili wake.

Mfuko uliokuwa na sehemu zingine za roboti huyo ulitoweka kwenye uwanja wa Frankfurt, hali iliyosababisha kufutwa kwa mkutano wa waandishi habari ambao ulipangiwa kufanyika jana Ijumaa, kwenye makavazi ya kitaifa mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Sophia iliyoundwa na kampuni ya Hong Kong, Hanson Robotics, imefanyiwa programu ya kuiwezesha kuzungumza lugha ya Amharic ambayo ni lugha rasmi nchini Ethiopia.

Sophia pia alitarajiwa kushiriki chakula cha jioni na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmes wakati wa ziara yake ya siku tatu.

Getnet Asefa, meneja wa mahabara ya Icog, iliyohusika na kutoa programu kwa Sophia anasema watamtafuta sehemu zingine.

Amharic ndiyo lugha ya kwanza ameweza kuzungumza baada ya kiingereza tangu aanze kuzungumza mwaka 2015.

Sophia hajaundwa kujibu maswali na badala yake atatumia teknolojia ya kujifunza kwa kusoma ishara za watu.

Alipata umarufu baada ya kuwa roboti ya kwanza kupata uraia wa nchi baada ya Saudi Arabia kumpa uraia mwaka uliopita.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>