Published On: Wed, Jun 13th, 2018

Mkurugenzi wa UNAIDS asema China inafanya kazi muhimu katika kupambana na UKIMWI

Share This
Tags

Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Kupambana na Ugonjwa wa Ukimwi la Umoja wa Mataifa UNAIDS Michel Sidibe amesema China inafanya kazi kubwa katika kupambana na ugonjwa huo.

Sidibe amesema hayo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, baada ya kutoa ripoti kuhusu kazi za Shirika hilo katika vita hiyo.

Amesema dunia nzima imepata maendeleo katika kutekeleza ahadi iliyokubaliwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2016, kuhusu “njia ya haraka” ya 2020 na kuelekea kutokomeza maambukizi ya ukimwi ifikapo mwaka 2030.

Amesema China inaichukulia elimu kuwa kazi kuu na kuhakikisha kuwa mfumo wa afya, mazingira, michezo na masuala mengine yanashughulikiwa.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>