Published On: Wed, Jun 13th, 2018
Business | Post by jerome

Kilimo cha matunda na mboga chakadiriwa kuajiri watu milioni 2.4 nchini

Share This
Tags

Kilimo cha matunda na mboga kinakadiriwa kuajiri watu milioni 2.4 nchini Tanzania,wengi wao wakiwa ni wanawake.

Hayo yamebainishwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara ,na Uwekezaji Stella Manyanya.

Manyanya amesema serikali imekuwa ikiweka kipaumbele katika kutambua fursa za masoko ya matunda na mboga ndani na nje ya nchi.

Amesema serikali kwa kushirikiana na Tanzania Horticulture Association (TAHA),imeandaa mafunzo kwa wakulima wa matunda na mboga kutoka mikoa ya Arusha,Kilimanjaro,Morogoro,Iringa,Njombe,Mbeya,na Zanzibar na inaendesha mafunzo ya kilimo bora cha bidhaa hizo ili kukidhi matakwa ya masoko ya ndani na nje ya nchi.

Aidha amesema mafunzo hayo pia yatafanyika katika mikoa iliyobaki ili kuwasaidia wakulima wa nchi nzima kupata soko la ndani na nje ya nchi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>