Published On: Thu, Jun 14th, 2018

FAMILIA 48 ZAKOSA MAKAZI BUHANDA-KIGOMA

Share This
Tags

Jumla ya familia saba zenye watu 48 zimekosa makazi na kulazimika kulala nje kwa zaidi ya wiki moja sasa katika manispaa ya Kigoma Ujiji katika eneo la Buhanda.

Hali hiyo imejitokeza baada nyumba zao kuvunjwa na kuamriwa kuondoka, kwamba ni mali ya taasisi ya Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu.

Baadhi ya wahanga akiwemo HARUNA SADICK GWALE wameelezea kadhia hiyo na kusema ni jambo lililowashtua kwani hakukutolewa notisi yoyote kabla ya nyumba zao kuvunjiwa.

SAUDA HAMIMU naye ni mmoja wa wahanga wa tukio hilo ambaye amesema mbali na adha wanayoipata, pia wameshindwa kutekeleza ibada ya mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Akizungumzia suala hilo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji BROWN NZIKU, amekiri nyumba takribani 22 zilizokuwa kwenye kiwanja namba 718 zimevunjwa, na kwamba kiwanja kilikuwa na mgogoro kati ya baadhi ya wananchi na taasisi ya Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislam.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>