Published On: Mon, Jun 11th, 2018

DORICE MOLLEL FOUNDATION YAENDELEZA JITIHADA ZA KUPUNGUZA WATOTO NJITI

Share This
Tags

Imeelezwa kuwa takwimu za shirika la afya duniani WHO, zinaonyesha kati ya watoto 10 wanaozaliwa kila siku hapa nchini, upo uwezekano kwamba mtoto mmoja huzaliwa akiwa njiti.

Takwimu hizo zimebainishwa jijini Dar es salaam na mkurugenzi wa afya ya mama na mtoto Dkt AHMED MAKUWANI wakati wa mkutano uliolenga kujadili mpango wa kuongeza likizo ya uzazi kwa wazazi wenye mtoto njiti.

Dk. MAKUWANI akimwakilisha waziri wa afya UMMY MWALIMU katika mjadala ambao umeandaliwa na taasisi ya DORIS MOLLEL amesema kati ya watoto wachanga 100 wanaozaliwa kila siku, watoto 25 hufariki dunia kulingana na sababu mbalimbali.

ALVARO RODRIGUEZ ni mwakilishi mkazi wa umoja wa mataifa nchini, kwenye mjadala huo amesisitiza juu ya umuhimu wa kuweka uangalizi kwa watoto wanaozaliwa wakiwa njiti, huku akiwakumbusha watunga sera.

Nae mwanzilishi wa taasisi ya DORIS MOLLEL, akizungumza kwenye mkutano huo, ameweka turufu yake kwa waziri mwenye dhamana na masuala ya afya, akidai pendekezo hilo huenda akalisikia na kulifanyia kazi.

Kwa sasa baadhi ya mataifa ulimwenguni yamefanikiwa kuongeza likizo ya uzazi kwa wazazi wenye watoto njiti, ambapo hatua hiyo imeongeza ufanisi wa malezi kwa watoto hao.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>