Published On: Wed, Jun 13th, 2018

Disco toto marufuku Eid El Fitri-RPC Tanga

Share This
Tags

Jeshi la polisi mkoani Tanga limepiga marufuku wamiliki wa kumbi za starehe kuendesha disco toto katika sherehe za Eid el Fitr na kusisitiza kuwa atakaye kiuka agizo hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Kamanda wa polisi mkoani Tanga EDWARD BUKOMBE  ametoa  agizo  hilo kwa  kuitahadharisha  jamii,  kufuatia historia  juu ya watoto kupoteza maisha hususan msimu wa sherehe za kidini katika kumbi za starehe.

Katika salamu zake za  Eid el Fitr kamanda BUKOMBE  ameitaka jamii kila mmoja kuwa mlinzi wa  nyumba yake na mali zake na kusisitiza kuwa wasisite kuwafichua  watenda maovu huku akiwatoa hofu wananchi kuwa jeshi hilo liko imara.

Nae  Sheikh wa mkoa wa Tanga  Alhajj Juma Liuchu amewaasa waislamu kuendeleza matendo mema katika kipindi   chote cha  uhai wao, wadumishe amani ya nchi  na  kusherehekea  vema skukuu ya Eid el Fitr .

Amesema Skukukuu ya Eid El Fitri  hutegemea mwandamo wa mwezi  na kuwashauri waumini wa dini hiyo wajiandae kufunga mfungo sita ambao una umuhimu mkubwa kwa kila muislam.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>