Published On: Wed, May 9th, 2018
Sports | Post by jerome

Waziri Mwakyembe afungua Mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi

Share This
Tags

Timu za majeshi kupitia michezo mbalimbali zimetakiwa kuweka mikakati na kuibua wanamichezo wazuri ambao wataiwakilisha vyema nchi katika mashindano ya kimataifa na kuleta ushindi na medali mbalimbali kama ilivyokuwa hapo zamani.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa ufunguzi wa muhula wa tano wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) katika uwanja wa uhuru jana Jijini Dar es Salaam

“Ni matarajio yangu kuwa uwepo wa michezo hii inaashiria azma na nia thabiti ya kurejesha enzi  za majeshi yetu kutoa uwakilishi ulio mzuri katika michezo ndani na nje ya nchi kama ilivyokuwa hapo zamani” amesema Mhe. Mwakyembe

Kwa upande wake Mnadhimu Mkuu Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed amesema kuwa kufanyika kwa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi kila mwaka kunathibitisha azma ya JWTZ kukuza na kuendeleza sekta ya michezo nchini kwa kuunda timu za JWTZ zitakazotumika kuimarisha timu mbalimbali za Taifa katika mashindano ya Kimataifa.

Jenerali Yakubu amesema kuwa uwepo wa michezo ya majeshi katika jumuiya ya Afrika Mashariki umekua nyenzo ya kudumisha amani baina ya nchi wanachama hivyo wachezaji watakaopata fursa kushiriki michuano hiyo washiriki vema na kuleta tija kupitia michezo hiyo.

Mashindano ya Muula wa tano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) yenye kauli mbiu isemayo “Tushiriki Michezo kama sehemu ya kazi, Kulinda   Afya zetu na kudumisha mshikamano yataendana na uteuzi wa wanamichezo watakaoteuliwa kuunda timu za JWTZ zitakazoshiriki mashindano tarajiwa ya Majeshi kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki huko nchini Kenya mwaka 2019

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>