Published On: Thu, May 17th, 2018

WATANZANIA WATAKIWA KUONDOA HOFU YA AJIRA ZA WAGENI

Share This
Tags

Waziri mkuu KASSIM MAJALIWA amesema serikali ipo makini na ajira za wageni na itaendelea kuhakikisha Watanzania wanapewa fursa kwanza.

Waziri mkuu ametoa kauli hiyo leo Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwake wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu LEAH KOMANYA aliyetaka kupata kauli ya Serikali juu ya wageni wanaoingia nchini na kupata ajira kwenye maeneo nyeti kama vile bandarini au viwanja vya ndege.

Akifafanua zaidi Waziri Mkuu amesema pale ambapo italazimu raia wa nje apate ajira, serikali itaendelea kusimamia ili kuhakikisha kama kweli nafasi hiyo haina mtu na ni nafasi nyeti yenye utaalam ambao hakuna mtanzania mwenye uwezo nayo.

Akijibu hoja kuhusu wageni kufanya kazi kwenye maeneo nyeti, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kuhakikisha kwamba hakuna mgeni anayefanya kazi kwenye maeneo ya viwanja vya ndege, bandari au yale ya mipakani.

Amesema endapo atakutwa mtu yeyote wa Taifa la nje anafanya kazi kwenye maeneo hayo, basi atakuwa ameajiriwa na kampuni ambayo inafanya shughuli maalum kwenye eneo hilo na kwa masharti yale yale kwamba watapata nafasi ya kufanya kazi kwenye kampuni hiyo kama nafasi hiyo hakuna mtanzania mwenye uwezo nayo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>