Published On: Thu, May 17th, 2018
World | Post by jerome

WARUNDI WAPIGA KURA KUAMUA MUHULA WA RAIS KUONGEZWA

Share This
Tags

Burundi inafanya kura ya maamuzi inayopania kuongeza muhula wa rais kutoka miaka tano hadi saba.

Marekebisho hayo ya katiba yakiidhinishwa na wananchi huenda rais PIERRE NKURUNZIZA akaongoza taifa hilo hadi mwaka 2034.

Lakini kampeni hizo zimechafuliwa na tishio za upinzani kususia kura hiyo ya maamuzi na pia madai kwamba serikali imekuwa ikiwatisha wafuasi wa upinzani.

Umoja wa mataifa unahofia huenda ghasia zikazuka baada ya mauaji ya watu 26 hivi majuzi.

Wiki iliyopita washambuliaji ambao serikali imewataja kuwa magaidi, walivamia jiji la Chibitoke wakafanya mauaji ya kiholela na kuaminika kutorokea nchini Congo.

Serikali inaamini kuwa walikuwa wanajaribu kukomesha kura ya maoni kwa kutia watu woga na kuvuruga amani.

Hali hii ikiendelea huenda warundi wengine wasipige kura kwani ni kura tata yenye matokeo makubwa.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>