Published On: Wed, May 16th, 2018
World | Post by jerome

Wapalestina wazika maiti 60 za watu waliouliwa na Israel

Share This
Tags

Maelfu ya wakaazi wa Gaza wamejitokeza hapo jana kuomboleza vifo vya Wapalestina wenzao 60 waliouawa Jumatatu na wanajeshi wa Israel katika maandamano ya wiki kadhaa na yaliyoanza tokea Machi 30.

Maandamano hayo ya Jumatatu yaliambatana na kufunguliwa kwa ubalozi wa Marekani mjini Jerusalem, hatua iliyowakasirisha Wapalestina na kukemewa na jumuiya ya kimataifa.

Uingereza na Ujerumani hapo jana zimetoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kujitegemea dhidi ya mauaji hayo. Na Baraza la Kulinda Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa litaitisha kikao maalumu hapo Ijumaa ijayo, kujadili jinsi hali ya haki za binadamu inayozidi kuwa mbaya katika maeneo ya Wapalestina, baada ya Israel kuwauwa Wapalestina 60 katika maandamano hayo ya Jumatatu.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>