Published On: Thu, May 17th, 2018
Business | Post by jerome

WAONYWA KUTOPANDISHWA BEI ZA VYAKULA KATIKA MFUNGO WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN

Share This
Tags

Wakati waumini wa dini ya kiislamu wakiwa wameanza funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani leo, wafanyabiashara wa vyakula mkoani Morogoro wametakiwa kuuza vyakula kwa bei  za kawaida  ili kuwawezesha waislamu kumudu gharama za mahitaji ya mfungo.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro DR. KEBWE STEVEN amesema kuna baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu hutumia  msimu huu kupandisha bei ya vyakula maradufu huku kamanda wa polisi mkoani Morogoro SACP URLICH MATEI, akiwahakikishia  usalama waislamu katika kipindi chote.

Nao Baadhi ya wafanyabiashara wa  kuuza vyakula vinavyotumika kipindi cha mfungo wakiwemo MARY MOSES  na LUCY YOHANA wamesema  kupanda kwa bei ya vyakula kunatokana  na wafanyabishara  na wakulima wengine kuwa na tamaa ya kutaka kujinufaisha.

Kwa upande wa Kaimu sheikh wa wilaya ya Morogoro ALHAJI MASENGA  amewasihi watu wote kuheshimu na kuutumia  vizuri mwezi huu wa toba kwa kufanya mema ili mwenyezi Mungu awasamehe dhambi zao

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni moja ya nguzo tano za uislamu ambapo kila mwaka waislamu wamekuwa wakifunga katika kipindi cha mwezi mmoja.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>