Published On: Wed, May 16th, 2018
Science | Post by jerome

Wanasayansi wafanikiwa kuhamisha kumbukumbu baina ya konokono

Share This
Tags

Kuhamishwa kwa kumbukumu kimekuwa ni kitu ambacho hakijafanikiwa kisayansi kwa miongo kadha lakini sasa huenda jambo hilo likapata ufumbuzi.

Kundi moja la wataalamu limefanikiwa kuhamisha kumbukumbu ya kijenetiki inayofahamiaka kama RNA kutoka kwa konokono mmoja kwenda kwa mwingine.

Kwanza konokono hao walipewa mafunzo ya kuwa na kinga fulani.

Wakati RNA iliwekwa kwa konokono ambao hawakuwa wamepewa mafunzo kama hayo, walionyesha tabia fulani.

Utafiti huo uliochapishwa kwenye jarida la eNeuro, unaweza kuwa mwanzi wa ugunduzi mpya kuhusu kuhamishwa kwa kumbukumbu ya akili.

Wanasayansi walitoa RNA kutoka kwa mfumo wa ufahamu wa konokono ambao walipata mshtuko na kudungwa RNA kutoka kwa konokono ambao hawakuwa hawakufunzwa kuwa na tabia fulani.

Konokono ambao hawakuwa na tabia fulani ambao walidungwa RNA kutoka kwa konokono walioshtuka, walionyesha tabia ya wale konokono RNA ilitolewa na kushtuka kwa karibu sekunde 40.

Prof David Glanzman, mmoja wa waandishi kutoka chuo cha California, Los Angeles alisema matokeo hayo ni sawa na kwamba kumbukumbu ilihamishwa.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>