Published On: Wed, May 16th, 2018

Wanafunzi wa shule ya msingi Mitambo Mtwara wapata vyumba vya madarasa

Share This
Tags

Baada ya kusota kwa kipindi kirefu wakiwa chini ya miti na katika vibanda vya nyasi kuitafuta elimu wakichomwa na jua, hatimae wanafunzi wa shule ya msingi Mitambo katika halmashauri ya wilaya ya Mtwara wameondokana na adha hiyo kwa kupata vyumba vya madarasa.

Wanasema ukiona mateso yanazidi basi ujue neema hukaribia, hakika ndivyo ilivyokua kwa wanafunzi 229 wa shule ya msingi Mitambo waliokua wanalazimika kusomea chini ya miti na katika vibanda vya nyasi kwa kukosa madarasa.

Leo hii jambo hilo limegeuka historia, baada ya serikali kuelekeza jitihada zake katika shule hiyo na kuamua kutumia takribani miezi Minne kukamilisha vyumba viwili vya madarasa huku vingine vitatu vikiwa katika hatua za mwisho na kuwafanya wanafunzi wa shule hiyo kuwa na furaha

Kero ya kusomea nje haikuwa kwa wanafunzi peke yao, bali hata kwa walimu pamoja na wazazi wa wanafunzi hao.

Halmashauri ya wilaya ya Mtwara ina shule za msingi 67 zilizosajiliwa ambapo kati ya hizo, shule kumi zinakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>