Published On: Wed, May 16th, 2018

Waislamu wajiandaa kwa mfungo wa Ramadhan wiki hii

Share This
Tags

Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani unaanza Alhamisi wiki hii duniani kote, watu wenye imani ya dini ya Kiislamu watajizuia kula chakula na kunywa tangu kuchomoza mpaka kuzama kwa jua.

Malengo haya ni katika kutimiza nguzo za uislamu kwa kuswali na kujizuia ,wakati kipindi hiki kikitazamwa kama nafasi ya kujisafisha kiroho.

Waislam maeneo mbalimbali katika nchi za Afrika mashariki wanaedelea na maandalizi ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ,hatua ya muhimu ya kutimiza nguzo ya nne kati ya nguzo tano za dini hiyo.

Katika nchi nyingi hasa Afrika Mashariki na Kati, waumini wa dini hiyo wana wasiwasi wa kuongezeka kwa bei ya vyakula.

Mwezi wa 9 katika kalenda ya Kiislamu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao ni maarufu zaidi kutokana na ibada ya Saumu. Katika mwezi huu Waislamu hutakiwa kufunga kutoka asubuhi mpaka jioni katika kipindi ambacho hawatakiwi kula wala kunywa chochote.

Mwezi wa Ramadhani ni muhimu kwa Waislamu kwa kuwa ndio mwezi ulioteremshwa Qoran na pia hufahamika kama mwezi wa kusoma zaidi Qoran.

Mbali na kujiepusha na kunywa na kula Muislamu hutakiwa kujiepusha na maovu na matendo ya dhambi na kuongeza katika matendo ya ibada kama swala, kusoma Qoran, kutoa sadaka na kadhalika.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>