Published On: Wed, May 16th, 2018

Waendesha bodaboda Bukoba wahofia kuuawa.

Share This
Tags

Hofu ya kuuawa kikatili kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana imetanda kwa waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda mjini Bukoba, baada ya madereva wa bodaboda watatu kuuawa kwa mtindo unaofanana ndani ya wiki moja iliyopita.

Kusafirisha abiria kwa kutumia pikipiki, ni biashara iliyoibuka kwa miaka ya hivi karibuni katika maeneo mbalimbali hapa nchini, na kupewa jina ambalo limezoa umaarufu kama Bodaboda.

Shughuli hii hufanywa na vijana wengi kwa lengo la kujiingizia kipato,lakini mkoani Kagera hali imekuwa tofauti kwani wengi wanahofia maisha yao kutokana na wenzao watatu kuuwawa  kikatili ndani ya wiki moja iliyopita.

Kinachoskitisha na kuacha maswali mengi kwa wakazi wa Bukoba ni wauaji hao kutochukua kitu chochote baada ya kufanya unyama huo.

Mkuu wa mkoa huo meja jenerali mstaafu Mustapha salum kijuu, licha ya kulaani na kusikitishwa na vitendo hivyo,amesema kuwa tayari uchunguzi umeshaanza kufanyika na watahakikisha watekelezaji wa mauaji hayo wanakamatwa.

Mauaji hayo ambayo yameleta hofu kwa wakazi wa Bukoba yameanza tena ikiwa ni miaka mitatu imepita tangu kutokea kwa mauaji ya kukata watu koromeo ambapo wauaji hao walitiwa mbaroni.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>