Published On: Wed, May 16th, 2018
World | Post by jerome

Uturuki yamuamuru balozi mdogo wa Israel kuondoka nchini

Share This
Tags

Uturuki imemtaka balozi mdogo wa Israel mjini Istanbul kuondoka nchi humo kwa muda, likiwa tukio la karibuni la kulipizana kisasi, kuhusiana na mgogoro unaozidi kufuatia hatua ya Israel ya kuwapiga risasi na kuwauwa wapalestina katika mpaka wa Gaza.

Tayari Uturuki binafsi imeshamtaka Balozi wake mjini Tel Aviv na balozi mdogo mjini Jerusalem kurudi nyumbani kwa mashauriano na kumtaka balozi wa Israel mjini Ankara naye kuondoka.

Uturuki imeelezea kusikitishwa kwake na mauaji ya Wapalestina 60 siku ya Jumatatu yaliofanywa na wanajeshi wa Israel, pamoja na kuikosoa hatua ya Marekani kuuhamishia ubalozi wake mjini Jerusalem kutoka Tel Aviv.

Rais wa Uturuki Recep Tayep Erdogan ameitisha mkutano wa kilele wa Jumuiya ya nchi za Kiislamu-OIC mjini Istanbul Ijumaa ijayo ambao anasema utatoa taarifa nzito kwa dunia, juu ya suala hilo. Wakati huo huo mataifa ya kiarabu yamelaani vikali mauaji ya Wapalestina katika mpaka wa Gaza.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>