Published On: Wed, May 9th, 2018
Business | Post by jerome

Utafiti: Tanzania yaorodheshwa miongoni mwa nchi uchumi utakua kwa kasi zaidi duniani

Share This
Tags

Tanzania imeorodheshwa kuwa miongoni mwa mataifa ambayo uchumi wake utakua kwa kasi zaidi kufikia mwaka 2026.

Kituo cha Kimataifa cha Maendeleo cha Chuo Kikuu cha Havard cha Marekani kinakadiria kwamba uchumi wa Tanzania utakuwa unakua kwa asilimia 6.15 wakati huo.

Tanzania itakuwa ya nne kwa uchumi wake kukua kwa kasi Zaidi kufikia wakati huo.

India ndiyo itakayoongoza kwa uchumi wake kukua kwa kasi ya 7.89 ikifuatwa na Uganda (7.46) na Misri ya tatu (6.63).

Makadirio ya ukuaji ya kituo hicho yalifanywa kwa kutumia Mchangamano wa Kiuchumi, kipimo kimoja ambacho huangazia uchangamano wa uzalishaji na uchangamano wa uwezo wa uzalishaji wa bidhaa za kuuzwa nje katika taifa Fulani.

Ripoti hiyo ya Havard ilibaini kwamba kampuni ambazo zimefanya mabadiliko chanya na kuingiza uchangamano katika sekta mbalimbali za uchumi kwa mfano India na Vietnam ndizo zitakazokua kwa kasi zaidi katika mwongo mmoja ujao.

Baada ya mwongo mmoja wa ukuaji wa kiuchumi ambao uliongozwa na mafuta na bei za bidhaa, watafiti wa Havard wamebaini kwamba mambo yamebadilika na sasa mataifa yenye uchumi unaotegemea sekta mbalimbali ndiyo yatakayofanya vyema Zaidi.

Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara, ukuaji wa kiuchumi ambao ulikuwa umeegemea mataifa ya magharibi mwa Afrika yaliyokuwa na mafuta pamoja na bidhaa sasa unaanza kuegemea zaidi Afrika Mashariki.

Baada ya Uganda na Tanzania, Kenya ni ya kumi katika orodha ya mataifa yanayotarajiwa kukua kwa kasi zaidi mwaka 2026 ambapo ukuaji wake utakuwa asilimia 5.87.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>