Published On: Sat, May 5th, 2018
Science | Post by jerome

Utafiti: Jinsi mwezi unavyoathiri usingizi wako

Share This
Tags

Katika kipindi cha miaka kadhaa iliopita , mwezi mkuu umelaumiwa kwa kusababisha kila kitu ikiwemo ongezeko la uhalifu, kusababisha kichaa mbali na ongezeko la wazazi wanaojifungua watoto.

Lakini je unaweza kuwa sababu ya baadhi yenu kushindwa kupata lepe la usingizi wiki hii?

Huenda sio vinjwaji ama hata muda uliochukua kutazama runinga ama kompyuta ambayo imekuweka macho.

Je kuna thibitisho la Kisayansi ?

Wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Basel nchini Switzerland walipata ushahidi wa ushawishi wa mwezi mkuu wakati walipofanya utafiti wa watu waliojitolea wanaolala katika maabara.

Matokeo yake yalionyesha kuwa wakati kuna mwezi mpevu watu 33 kati yao ambao walikuwa hawajui kuhusu lengo la utafiti huo na wasioweza kuona mwezi kutoka kwa vitanda vyao

  1. -Walichukua dakika tano zaidi kupata usingizi
  2. -Muda wa usingizi wao ulipungua kwa dakika 20
  3. -walipoteza asilimia 30 ya usingizi mzito.

Lakini cha kushangaza ni kwamba watafiti hao walisema kuwa sababu hiyo haitokani na mwangaza mwingi unaotoka katika mwezi huo kwa kuwa walilala katika vyumba vyenye giza totoro.

Maelezo sahihi kulingana na utafiti uliotolewa 2013 ni kwamba kuna uhusiano kati ya usingizi na mwezi mkuu.

Profesa Christen Cajochen , mtu aliyefanya utafiti huo anasema kuwa: kupatwa kwa mwezi kunaathiri usingizi hata wakati ambapo mtu hauoni mwezi na hajui mwezi huo ulivyo.

Je ni nini tunachoweza kufanya iwapo mwezi mkuu unaathiri usingizi wetu?

Kwa neno moja-Hakuna .

Mtaalam wa usingizi nchini UIngreza Dkt Neil Stanley amesema kuwa iwapo mwezi huo utaathiri usingizi wako kutokana na mwangaza wake basi kitu kitakachosaidia ni kuvaa kitambara kinachoziba macho .

Lakini utafiti huo wa 2013 unasema kuwa tatizo hilo halisababishwa na mwangaza.

Anasema kuwa utafiti huo ulizua hisia wakati ulipochapishwa lakini bado unafaa kufuatiliwa kwa karibu na uchunguzi wa watu wengi na kwa kipindi kirefu.

”Sio miongoni mwa yale maswala ambayo hayawezi kuaminika hivyobasi kupata athari zake ni muhimu sana”, alisema. he said.

Hatahivyo hakujakuwa na utafiti mwengine wowote uliofanywa baada ya utafiti huo.

Pia amesema kuwa iwapo watu wanaripoti kutopata usingizi mzuri baada ya mwezi mpevu huenda ni mfano wa kuthibitisha hilo.

Mwezi mpevu huathiri macho na watu wanauhusisha na kukosa usingizi huku mwezi mdogo ukionekana bila kusabbaisha athari.

”Miezi mikuu huandikwa katika shajara za watu. Kila mtu anaandika kuhusu miezi mikubwa siku hizi”, alisema.

Ni nini kingine unachofanya mwezi mkuu kulaumiwa?

Hadithi za zamani zinasema kuwa mwezi ,mpevu hutufanya kuwa wenda wazimu ama hata kutufanya kuwa mbwa mwitu.

Kuna ushahidi mwingi kuonyesha kuwa kuna ajali nyingi, visa vya ghasia na visa vya wenda wazimu wakati mwezi unaopopevuka.

Maafisa wa polisi mjini Brighton walilazimika kuwaandika kazi maafisa zaidi wa polisi wakati wa miezi mikuu 2007 baada ya kufanya utafiti na kubaini kwamba kuna visa vingi vya ghasia.

Hadithi nyingine ya zamani ni kwamba miezi mikuu huwafanya wanawake kujifungua.

Pia imesababisha watu kuumwa na wanyama, visa vingi vya kujitoa uhai mbali na kulala ukitembea. Lakini wanasayansi wamekosa ushahidi wa kutosha na wengi

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>