Published On: Tue, May 8th, 2018
Sports | Post by jerome

TP Mazembe yatuma salamu kwa El Jadidi

Share This
Tags

Mabingwa wa kombe la Shirikisho timu ya TP Mazembe imeanza vyema hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika baada ya kupata ushindi wa jumla ya magoli 4-1 dhidi ya ES Setif ya Algeria mchezo uliopigwa uwanja wa Frederic Kibassa Maliba mjini Lubumbashi.

Mazembe walikuwa wa kwanza kupata bao daikka ya 10 kupitia kwa mshambuliaji wao Likonza Malango Ngita, na dakika ya 23 aliongeza bao la pili kwa mkwaju wa penalti. Akitokea benchi Meshack Elias alipachika kimiani goli la tatu kabla ya Nathan Sinkala kukamilisha idadi ya magoli dakika ya 80. Bao la kufutia machozi la Setif lilifungwa na Nessakh.

Kwa matokeo hayo, Mazembe wanaongoza kundi B, wakifuatiwa na El Jadidi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>