Published On: Tue, May 15th, 2018

TARURA yakosolewa ubovu wa barabara kilolo Iringa

Share This
Tags

Baraza la Madiwani katika halmashauri ya wilaya kilolo wamelalamikia utendaji usioridhisha wa wakala wa barabara mijini na vijijini TARURA kutokana na ubovu wa miundombinu ya barabara zinazounganisha halmashauri hiyo na kusababisha adha kwa wananchi.

Walikua Wakizungumza katika kikao cha baraza hilo Wilayani Kilolo baada ya diwani wa kata ya Ihimbo kutaka baraza hilo kujadii hoja ya Ubovu wa miundombinu huku wakitilia shaka utendaji kazi wa chombo hicho kinachoshughulikia uboreshaji wa Miundombinu.

Kufuatia majadiliano ya madiwani yaliyodumu kwa takriban dakika 45 ikamlazimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya kilolo Aloyce Kwezi  na mkuu wa wilaya hiyo Asia Abdalah kumtaka Meneja wa TARURA  Kujitathmini na kufanya kazi kwa kuzingatia mahitaji ya halmashauri ili kupungua changamoto hizo pamoja na kurahisisha upitikaji wa njia hizo.

Halmashauri ya wilaya kilolo imekuwa ikikabiliwa na ubovu wa miundombinu ya barabara kwa muda mrefu licha ya kuwa na uzalishaji wa mazao ya biashara jambo ambalo limekuwa likikwamisha usafirishaji.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>