Published On: Wed, May 9th, 2018
Business | Post by jerome

Miradi 100 yasajiliwa kwa miezi 4 Tanzania

Share This
Tags

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimetoa ripoti ya robo mwaka ya hali ya uwekezaji nchini huku Tanzania ikionesha kushika nafasi ya tano miongoni mwa mataifa 10 duniani, ambayo uchumi wake unakua kwa kasi.

Akitoa ripoti hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Geofrey Mwambe alisema kuimarika kwa hali hiyo ya uchumi, kunatokana na uhamasishaji unaoendelea kufanywa na TIC kupitia njia mbalimbali ikiwemo mikutano ya ndani na nje ya nchi kuhamasisha uwekezaji.

Alisema katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Aprili, mwaka huu Kituo hicho kimefanikisha uandikishaji wa miradi mipya 109 yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 13.3 inayotarajiwa kutoa fursa za ajira 18,172 kwa wananchi mbalimbali.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>