Published On: Wed, May 16th, 2018

Tangu kuanzishwa kwa Bunge la Afrika Mashariki mwaka 2001,jumla ya sheria 78 zimetungwa

Share This
Tags

Serikali imesema tangu kuanzishwa kwa Bunge la Afrika Mashariki mwaka 2001 hadi sasa jumla ya sheria 78 zimetungwa na kati ya hizo sheria 20 zimeridhiwa na wakuu wa nchi wanachama huku nyingine zikiwa zipo katika hatua mbalimbali za kusainiwa na kuridhiwa.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, BALOZI AUGUSTINE MAHIGA wakati akijibu swali la ALLY SALEHE Mbunge wa Malindi  aliyetaka kujua ni sheria ngapi zimetungwa tangu kuanzishwa kwa umoja huo.

BALOZI Dk. MAHIGA amesema sheria zilizotungwa zimelenga katika kuimarisha biashara kukuza uchumi baina ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuwezesha taasisi na vyombo vya jumuiya kutekeleza majukumu yake.

Katika swali la nyingeza mbunge wa Temeke ABDALA MTOLEA ametaka kujua njia zinazotumika kutangaza fursa ndani ya jumuia ya afrika mashariki na kuwafikia wananchi wa vijijini.

 

Katika hatua nyingine serikali imesema hadi  kufika  Machi 2018  jumla ya shilingi  bilioni 182.92 sawa na asilimia  32.89 ya makadirio  ya shilingi  bilioni 556.08  kimepokelewa  kutoka  kwa washirika wa maendeleo  kwa mwaka  wa fedha 2017/2018.

Naibu Waziri wa Fedha  na Mipango Mh Dk.Ashantu Kijaju wakati akijibu  swali la  Mh MACHANO OTHUMAN kutoka Baraza La Wawakilishi Zanzibar aliyetaka kujua   ni kiasi gani cha fedha kutoka Basket Fund  kimepatikana kwa mwaka 2017/2018.

PIA Waziri wa mifugo na uvuvi LUHAGA MPINA akitoa taarifa bungeni amewatoa hofu watanzania juu ya sakata la mizoga kukutwa kwenye gari tegeta jijini Dar es salam ambapo amesema viongozi ngazi zote wapo makini na hakuna mtanzania atakayekula kibudu.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>