Published On: Thu, May 17th, 2018

TANAPA YAZINDUA MPANGO WA UENDESHAJI WA UHIFADHI ILI KUBORESHA UTENDAJI

Share This
Tags

Shirika la Hifadhi za Taifa, TANAPA, limezindua mpango wa uendeshaji wa uhifadhi wa miaka kumi katika hifadhi ya taifa ya milima ya Mahale iliyopo mkoani Kigoma, utakaosaidia masuala mbalimbali ya kiutendaji ili kuongeza tija na kuifanya hifadhi hiyo kutambulika zaidi kwa uhifadhi wanyama aina ya Sokwe.

Kaimu Mkurugenzi wa TANAPA ambaye ni Meneja Ujirani mwema wa shirika hilo AHMED MBUGI, amesema mpango huo utaisaidia hifadhi ya milima ya Mahale kujitegemea na kuleta tija kwa wawekezaji katika hifadhi hiyo na  pia kuongeza pato la taifa kutokana na sekta ya utalii nchini.

Katika uzinduzi wa mpango huo uliofanyika mjini Kigoma, Mkuu wa Mkoa huo Brigedia Jenerali Mstaafu EMMANUEL MAGANGA, amesema ipo haja ya serikali kuanzisha kituo cha utalii mkoani humo, kutokana na mkoa kuwa na vivutio vingi ambavyo havipo mahali pengine duniani.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>