Published On: Wed, May 9th, 2018
Business | Post by jerome

Tabora yaongoza kwa uzalishaji wa mbegu bora ya pamba.

Share This
Tags

Zao la pamba mkoani Tabora limetajwa kufanikiwa kwa asilimia sabini na tano kutokana na uzalishaji wa mbegu kwa msimu huu wa mwaka 2018 na kuvuka malengo kutoka tani 850 hadi kufikia tani 15,600.

Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri  akizungumza na wadau wa pamba  katika kikao cha tathmini ya uzalishaji wa mbegu  wilayani Igunga amesema kutokana na uzalishaji huo wa mbegu serikali imeahidi kujenga kiwanda cha pamba wilayani Igunga ili kuleta tija kwa wakulima wa zao hilo.

Aidha Mwanri, amewaagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wanasimamia vyama vya ushirika vya wakulima wa zao  hilo hali itakayowasaidia kuingia katika mfumo wa kilimo cha kisasa.

Serikali katika kulipa kipaombele zao hilo la pamba  tarehe mosi mwezi mei ilizindua soko la ununuzi wa zao hilo nchini.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>