Published On: Wed, May 9th, 2018
Sports | Post by jerome

Mashindano ya CECAFA Wanawake ya Rwanda mwezi huu yaahirishwa

Share This
Tags

Mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika Mashariki na kati kwa timu za wanawake yaliyopangwa kufanyika nchini Rwanda kuanzia Mei 12 hadi Mei 22 mwaka huu yameahirishwa.

Tangazo la kuahirishwa limetolewa na Shrikisho la mpira wa miguu la Rwanda FERWAFA, kwa madai ya kukosekana fedha kwa ajili kuendeshea mashindano hayo.

Awali Baraza la vyama vya soka ngazi ya kanda CECAFA, lilitangaza kutoa pesa kwa ajili ya uendeshaji, lakini kwa mujibu FERWAFA, baraza hilo halijatoa fedha zozote na wala halijafanya mawasiliano yoyote mpaka sasa zikiwa zimesalia siku chache tarehe ya kuanza mashindano ifike.

Katika hatua nyingine Rwanda imevunja kambi ya timu yake iliyoanza wiki moja iliyopita.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>