Published On: Thu, May 17th, 2018

SERIKALI KUSAJILI NA KUTOA LESENI ZA BIASHARA KWA NJIA YA MTANDAO

Share This
Tags

Serikali imeamua kusogeza huduma ya usajili wa biashara na utoaji leseni za biashara karibu na wananchi, kwa kuanzisha mfumo mpya wa usajili na kutoa leseni za biashara kwa njia ya mtandao.

Hatua inatajwa kuboresha mazingira ya biashara nchini.

Hapo awali wananchi wenye nia ya kuanzisha biashara walilazimika kusafiri umbali mrefu kwenda mpaka jijini Dar es Salaam ili kusajili majina ya biashara, lakini kwa mfumo huu mpya wataweza kusajili biashara zao katika maeneo waliyopo.

Hayo yameelezwa na Meneja Uboreshaji Mazingira ya Biashara kutoka Baraza la Taifa la Biashara WILLY MAGEHEMA, wakati wa kutoa mafunzo ya usajili na utoaji leseni za biashara kwa njia ya mtandao kwa maafisa biashara na wataalam wa TEHAMA, kutoka wilaya zote za mkoa wa Kigoma.

Kwa upande wake Msaidizi wa Msajili Mwandamizi kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni BRELA, LUMAMBO SHIWALA amesema ili kusajiliwa katika mfumo huo mpya ni lazima anayesajiliwa awe na kitambulisho cha taifa.

Awali akifungua mafunzo hayo Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma CHARLES PALANGYO, ameagiza vituo vyote vya biashara vilivyojengwa katika wilaya zote mkoani humo, vitumike kwa malengo yaliyokusudiwa na maafisa biashara waeleweshwe vyema juu ya matumizi ya vituo hivyo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>