Published On: Thu, May 17th, 2018

SELIAN YAJA NA MPANGO MKAKATI WA SOKO LA UHAKIKA LA MBAAZI

Share This
Tags

Kituo cha utafiti wa kilimo cha Selian cha jijini Arusha kimekuja na mpango mkakati wa kuhakikisha  wakulima wanapata soko la uhakika kwa zao la Mbaazi  kwa kuzitaka taasisi mbalimbali kununua na kutumia zao hilo kama kitoweo.

Tayari wakulima wa zao hilo wamejizatiti kupigania upatikanaji wa soko la ndani kwa kuwataka watu kubadilika na kutumia mbaazi zaidi kuliko maharagwe

Mpango mkakati huo umekuja huku ikielezwa kwamba tani 75 hazikuvunwa  katika msimu uliopita na tani 90 zilivunwa lakini hazijauzwa hivyo kuwakatisha tamaa wakulima kuendelea kulima zao hilo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>