Published On: Wed, May 16th, 2018

Polisi Morogoro wakamata vipodozi vilivyopigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu

Share This
Tags

 

WATU  wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi   kwa tuhuma ya kukutwa na vipodozi vilivyopigwa marufuku   kwa matumizi ya binadamu na kukutwa  na pembe za ndovu  mkoani Morogoro

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wapolisi mkoani Morogoro

WATU  wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi   kwa tuhuma ya kukutwa na vipodozi vilivyopingwa marufuku   kwa matumizi ya binadamu na kukutwa  na pembe za ndovu  mokoani Morogoro

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wapolisi mkoani Morogoro SACP Ulrich Matei   amesema   mei kumi na tano mwaka huu   maeneo ya  Melela barabara kuu ya Iringa Dare-salam  askari polisi walifanya upekuzi katika gari  yenye namba za  usajili T. 877DWG aina ya Higher mali ya kampuni ya Princes Muro na kufanikiwa kukamata katoni hamsini na sita ya vipodozi ambavyo vimepigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu  vikiwa vimehifadhiwa katika mifuko miwili yaplastic , begi moja na boxi moja

Kamanda Matei amesema   baada ya kufanya upekuzi huo wamefanikiwa  kumkamata   kondakta wa gari hilo bw. Bibianna Mwita mkazi wa Kitunda  jijini Daresalam  ambavyo alikuwa anavisafirisha kutoka jijini Daresaalm kweda  jijini Mbeya kwa ajili ya kufanya biashara.

Katika hatua nyingine  jeshi hilo linamshikilia  Joel Amosi mkazi wa  Mikumi kwa kukutwa na pembe za ndovu mbili  zenye uzito wa kilogramu kumi  zenye thamani ya shilingi million thelathini na nne akiwa amevipakia kwenye baiskeli

Watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakani.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>