Published On: Wed, May 16th, 2018

Polisi Kilimanjaro wakimbizana na wasafirisha mirungi

Share This
Tags

POLISI mkoani Kilimanjaro kupitia kitengo chake cha kudhibii dawa za kulevya imefanikiwa kukamata gunia la Majani yenye uzito wa Kilogramu 48.8 yanayodhaniwa kuwa ni Dawa za kulevya aina ya Mirungi baada ya kutelekezwa na vijana wawili waliokuwa wakiwakimbia askari Polisi kwa kutumia pikipiki.

Ni takribani dakika 30 za hekaheka baina ya askari Polisi na vijana wanaodaiwa kusafirisha Dawa za kulevya aina ya Mirungi kutoka nchi jirani ya Kenya walipojaribu kuwakimbia askari hao kwa kutumia pikipiki huku wakiwa wamebeba gunia linalotajwa kuwa na Mirungi.

Askari Polisi wakiongozwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issa walitumia magari kuwafukuzia vijana hao hadi maeneo ya msitu wa Kilemaboro unaounganisha maeneo ya Shantytown na Kibosho ambapo walitelekeza mzigo huo wenye vifurushi mbalimbali.

Biashara ya dawa za kulevya aina ya Mirungi imekuwa ikishamiri kwa mikoa ya kaskazini nah ii ni kutokana na kupakana na nchi jirani ya Kenya ambapo kunatajwa kulimwa kwa wingi bila ya uwepo wa zuio la kisheria.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>