Published On: Tue, May 15th, 2018
Business | Post by jerome

Mradi wa umeme wa Mto Rufiji kuanza Julai

Share This
Tags

Waziri wa Nishati, wa Tanzania Dk Medard Kalemani amesema kazi ya ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme kwa nguvu za maji ya Mto Rufiji eneo la Stiegler’s Gorge, unatarajiwa kuanza Julai mwaka huu.

Dk Kalemani amesema kuwa hatua hiyo ya kuanza kwa mradi inatokana na kazi ya tathmini ya kumpata mkandarasi wa ujenzi kukamilika.

Akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dk Kalemani amesema mradi huo utaanza baada ya taratibu zote za kiutendaji kukamilika, ambako mradi huo mkubwa wa umeme utaongeza megawati 2,100, zaidi ya megawati 560 zinazozalishwa katika miradi mingine ya maji.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>