Published On: Mon, May 14th, 2018

MOJA YA VIBOKO WATATU TISHIO TANGA AUAWA

Share This
Tags

Kiboko mmoja kati ya watatu waliokuwa wanatafutwa na jeshi  la majini ambao wanahatarisha  maisha ya  wananchi wa jiji la Tanga  amepatikana, katika mwambao mwa bahari ya Hindi  wilayani  Tanga  na kuuwawa.

Kwa  mara ya kwanza kiboko  walipoonekana katika bahari ya hindi  mkoani Tanga  walikuwa tishio kwa  wakazi  jijini humo hali iliyopelekea kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo hayo ambapo  wengine wawili wanaendelea  kutafutwa na jeshi hilo hapa katibu tawala wilayani Tanga anabainisha juu ya tukio hilo.

BERNARD GASPER  na  AYARI JUMA ni mashuhuda wa tukio ambao wamesema mnyama huyo ameuawa nchi kavu akiwa katika harakati za kukimbilia baharini.

Wananchi wa eneo hilo wameeleza furaha yao baada ya kiboko mmoja kuuawa kwani kitendo cha wao kuonekana, kulidhoofisha  juhudi za kujitafutia kipato.

Kiboko ni moja ya wanyama wenye uzito mkubwa kwani hufikia kilo 2,500 mpaka  3,400 ambaye hushika namba tatu  kati ya wanyama wenye uzito mkubwa akitanguliwa na tembo mwenye kati ya kilo 8,500 na13,000,   kifaru kati ya kilo 2,350 na  3,850 na ana uwezo wa kukimbia  kufikia  mita 48 kwa saa.

Wanyama hawa pia husadikiwa kuwa wametoka katika mbuga ya Saadan iliyopo mkoani Tanga.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>