Published On: Tue, May 15th, 2018
World | Post by jerome

Mazishi ya waliouawa Gaza kufanyika leo

Share This
Tags

Jeshi la Israel limesema ndege yake imeshambulia maeneo kadhaa yaliyolengwa ya chama cha Hamas katika ukanda wa Gaza, kama jibu la maandamano makubwa katika mpaka wake na Gaza.

Jeshi la Israel limesema maeneo 11 ya kigaidi katika kambi ya kijeshi ya Hamas yalishambuliwa huku vifaru vya kijeshi pia vikishambulia kambi mbili za Hamas katika ukanda huo. Kulingana na jeshi la Israel, waandamanaji walitumia vilipuzi na mabomu ya petroli dhidi ya wanajeshi wake na pia kuwa risasi zilifyatuliwa kwa wanajeshi wake walioko katika mpaka huo.

Rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan ameishutumu Israel na kusema inaendeleza kitendo cha kigaidi. Erdogan ameendelea kusema “Tumetangaza siku tatu ya kuomboleza nchini mwetu na tutashikamana na ndugu zetu Wapalestina.

Zaidi ya hayo tunaitisha mkutano wa dharura wa Jumuiya ya nchi za Kiislamu, nikiwa mwenyekiti wake wa zamu.” Wanajeshi wa Israel waliwaua Wapalestina 59 katika maandamano yaliyofanyika jana. Jeshi hilo limekadiria kuwa takriban Wapalestina 40,000 walishiriki kwenye maandamano hayo.

Marehemu wanatarajiwa kuzikwa leo. Wakati huo huo Wapalestina leo wanakumbuka siku ya janga linalojulikana kama Nakba, yaani miaka 70 ya kutimuliwa kwao wakati wa kuundwa kwa Israel.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>