Published On: Thu, May 17th, 2018
Sports | Post by jerome

MASHABIKI WAICHANGIA NJOMBE MJI KUINUSURU KUSHUKA DARAJA

Share This
Tags

Katika kuinusuru klabu ya Njombe Mji kushuka daraja mashabiki na wapenzi wa timu ya simba mkoani humo wamefanya harambee na kuichangia klabu hiyo kiasi cha shilingi laki mbili na elfu kumi na tano.

Klabu ya Njombe ambayo ni kipenzi cha wananjombe imekuwa na mwenendo wa kusuasua tangu ligi ianze ambapo tatizo kubwa limekuwa likiripotiwa kuwa ni ukata wa fedha hali inayoifanya klabu hiyo kuwa na maandalizi ya chini ya kiwango katika michezo yake na kupelekea kupata matokeo mabaya.

Hadi sasa Njombe inashikilia mkia katika msimamo wa ligi kuu bara ikiwa na pointi 22, point moja nyuma ya ndanda na mbili nyuma ya majimaji ya mjini Songea huku zote zikiwa zimesaliwa na michezo miwili.

Kutokana na hali hiyo mashabiki wa timu ya simba wanaliona tatizo hilo na kuamua kuchangisha fedha zitakazosaidia kuipa nguvu timu hiyo kuelekea michezo iliyosalia kwa madai ya kwamba kusalia kwake kutaifanya simba na yanga kuendelea kwenda Njombe.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Njombe Mji mhasibu wa klabu hiyo NSAJIGWA MWAKIGOBE wakati wa makabidhiano ya fedha hizo amesema kitendo kilichofanywa na mashabiki wa timu ya simba kinaonyesha  uzalendo mkubwa na kuwatoa hofu wapenzi wa Njombe kwamba watapambana kwa kila hali ili kuinusuru timu hiyo

Njombe Mji inahitaji kushinda michezo yote miwili ukiwemo wa wa tarehe 25 dhidi ya mtibwa na tar 28 dhidi ya mwadui huku maombi mengi yakielekezwa kwa wapinzani wake ndanda na majimaji kupoteza baadhi ya michezo yake.

Joto la michezo hiyo linakigusa chama cha mpira Njombe (NJOREFA) ambacho kimewaomba wananjombe kujitokeza kwa wingi katika michezo iliyosalia ili kuwapa hamasa wachezaji.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>