Published On: Tue, May 15th, 2018
World | Post by jerome

Maandamano zaidi kushuhudiwa Gaza leo Jumanne

Share This
Tags

Maandamano mapya dhidi ya Israel yanatarajiwa huko Palestina leo Jumanne, siku moja baada ya wanajeshi kuwaua watu 58 huko ukanda wa Gaza.

Jumatatu ilikuwa siku mbaya zaidi tangu maandamano kuanza kwenye mpaka wa Gaza wiki saba zilizopita.

Leo itakuwa ni maadhimisho ya miaka 70 ambayo Wapalestina wanayataja kama Nakba – ambayo ni maadhimisho ya kuhamishwa kwa Wapalestina kufuatia vita vya kuundwa kwa Israel.

Msukosuko mpya unatarajiwa huko Gaza siku ambayo yatafanyika maziko ya wale waliouawa.

Ghasia za Jumatatu zilizuka wakati ambapo Marekani ilikuwa inafungua ubalozi wake huko Jerusalem hatua iligadhabisha wapalestina.

Wanadai Jerusalem Mashariki ni mji mkuu wa taifa la baadaye la Palestina na kuitaja hatua ya Maeekani kama inayounga mkono Israel kuweza kudhibiti mji huo wote inaoutaja kuwa mji wake mkuu.

Maafisa wa Palestina wanasema takriban watu 2,700 walijeruhiwa wakati wa ghasia hizo siku ya Jumataua – zilizo mbaya zaidi kuwai kushuhudiwa huko Gaza tangu mwaka 2014.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema jeshi lake lilikuwa linajilinda dhidi ya watawala wa Gaza, Hamas ambao anasema lengo lako ni kuiangamiza Israel.

Israeli PM Benjamin Netanyahu said his military was acting in self-defence against Gaza’s Islamist rulers, Hamas, who he said wanted to destroy Israel.

Kipi kilitokea mpakani?

Wapalestina walikuwa wanaandamana siku ya Jumatatua jinsi wamekuwa wakiandana kwa wiki sita katika sehemu ya maandamano yaliyochochewa na Hamas yanaofahamika kama “Great March of Return”.

Hata hivyo yale ya Jumatatua na leo Jumanne yanakwenda sambamba na maadhimisho ya kuundwa taifa la Isreal mwaka 1948 na kuhama maelfu ya wapalestina kutokana na vita vilivyofuatia.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>