Published On: Wed, May 16th, 2018
World | Post by jerome

Kura ya maoni kuhusu mabadiliko ya katiba kupigwa Alhamisi hii nchini Burundi

Share This
Tags

Wananchi wa Burundi wanapotarajiwa kupiga kura ya maoni hapo kesho kuirekebisha Katiba, wengi wanaamini kuwa mabadiliko yatakayofanyika yatampa rais Pierre Nkurunziza kuendeleza kuongoza hadi mwaka 2034.

Katiba ya sasa iliyokubaliwa mwaka 2005, ililenga kuleta amani katika taifa hilo la Afrika ya Kati na kuweka usawa wa kikabila katika nyanja mbalimbali ili kuepuka vita vya miaka ya tisini kati ya Wahuu na Watutsi.

Miongoni mwa mabadiliko ni pamoja na kuwepo kwa mihula miwili ya miaka saba kwa rais kudumu badala ya mihula miwili ya miaka mitano.

Iwapo wananchi wa Burundi watafanya mabadiliko hayo hapo kesho, rais Nkurunziza huenda akawania tena urais mwaka 2020.

Pamoja na hilo, mabadiliko yanayopendekezwa ni pamoja na mamlaka makubwa kuwa mikononi mwa rais kuunda nafasi ya Waziri Mkuu huku wadhifa wa makamu mmoja wa rais ukiondolewa.

Katiba ya sasa inataka mamlaka kugawanywa kati ya rais na Makamu wawili wa rais.

Waziri Mkuu atapewa mamlaka ya kusimamia shughuli za serikali.

Hata hivyo, kama ilivyo kwenye Katiba ya sasa, asilimia 60 ya wabunge na serikali ni lazima wawe kutoka katika kabila la Wahutu huku asilimia 40 ikiwaendelea Watutsi.

Hata hivyo, Bunge la Seneti linaweza kubadilisha mfumo huo wa uongozi.

Wanasiasa wa upinzani wengi wanaoishi nje ya nchi hiyo, wanapinnga mabadiliko haya ya Katiba na wamewaambia wananchi wa upinzani kupiga kura ya Hapana kwa sababu yanavunja mkataba wa amani wa Arusha uliomaliza vita vilivyodumu zaidi ya mwongo mmoja nchini humo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>