Published On: Wed, May 16th, 2018
Sports | Post by jerome

Klabu Bingwa Afrika: KCCA ya Uganda yaishinda Al Ahly ya Misri 2-0

Share This
Tags

x-default

Klabu ya KCCA ya Uganda jana imepata ushindi wa kihistoria dhidi ya klabu bora kabisa barani Afrika ya Al Ahly ya Misri kwenye mechi ya raundi ya pili ya hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika.

Magoli mawili ya timu hiyo yalipatikana kupitia Saddam Juma na Timothy Awany aliyefungwa kwa njia ya penati.

Nafasi mbili za kusawazisha walizopata Al Ahly zilikataliwa na golikipa wa KCCA Charles Lukwago aliyetimiza wajibu wake kwa kupangua penati katika kipindi cha kwanza na kuuzia baadhi ya mipira iliyopigwa na nyota wa kutumainiwa wa Misri kwenye mechi hiyo. Kwa ushindi huo sasa, KCCA inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi A, nyuma ya Esperance ya Tunisia yenye alama nne baada ya kupata ushindi wa magoli 4-1 ilipocheza dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>