Published On: Tue, May 15th, 2018

Kituo cha mabasi yaendayo mikoani mjini Musoma chajaa maji

Share This
Tags

Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Mara zimepelekea kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha mjini musoma kujaa maji na hivyo abiria na wamiliki wa magari ya abiria kulalamikia hali hiyo, licha ya kulipa ushuru kila siku lakini halimashauri ya manispaa ya musoma imeshindwa kufanya marekebisho ya miundombinu katika kituo hicho ambacho kinadaiwa kujengwa kwa zaidi ya shilingu bilioni mbili.

Baadhi ya abiria na wasafirishaji wa abiria katika kituo hicho kilichopo maeneo ya bweri,wamesema kuwa kutokana na kituo hicho kutokamilika kumesababisha kuwepo na madimbwi makubwa ya maji na licha ya kutoa malalamiko katika halimashauri hiyo,lakini hadi sasa hakuna hatua ambazo zimechukuliwa kurekebisha hali hiyo

 

Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Musoma John Masero,mbali na kukiri kituo hicho cha mabasi kujengwa chini ya kiwango kwamba hivi sasa halmashauri hiyo imeweka mipango ya kujenga upya stendi hiyo lakini pia akawataka wananchi kuwa na subira wakati swala hilo linatafutiwa ufumbuzi ili kuondoa kero hiyo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>