Published On: Wed, May 2nd, 2018

Kanye West asema Wamarekani Waafrika ‘walipendelea’ kuwa watumwa

Share This
Tags

Msanii wa muziki wa Rap nchini Marekani Kanye West amesema kuwa utumwa wa Wamarekani Waafrika uliofanyika zaidi ya miaka 100 iliopita lilikuwa chaguo lao.

‘Unaposikia kwamba utumwa ulifanyika kwa zaidi ya miaka 400.. miaka 400? ni kama walipendelea hilo kufanyika’, alisema katika tovuti ya burudani ya TMZ.

Nyota huyo hivi karibuni aligonga vichwa vya habari kwa kumuunga mkono rais Donald Trump.

Watu weusi walilazimishwa kutoka Afrika na kuelekea Marekani katika karne za 17, 18 na 19 na kuuzwa kama watumwa.

West baadaye alituma ujumbe wa Twitter na kusema kwamba hakueleweka vyema na kwamba alizungumza kuhusu miaka 400 kwa sababu ‘fikra zetu’ haziwezi kufungwa kwa miaka mingine 400.

Katika mahojiano na TMZ West alisema hivi sasa tunachagua kufanywa watumwa swala lililozua hisia kali kutoka kwa mfanyikazi mmoja mweusi katika kampuni hiyo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>