Published On: Wed, May 16th, 2018
Business | Post by jerome

Indonesia kujenga kiwanda cha nguo Simiyu

Share This
Tags

Nchi ya Indonesia inatarajia kuwekeza mkoani SIMIYU kwa kujenga kiwanda kikubwa cha kutengeneza nguo kutokana na mkoa huo kuzalisha kiasi kikubwa cha pamba.

Hayo yamesemwa kwa nyakati tofauti  wilayani  BARIADI na MASWA kwenye ziara  ya balozi wa Indonesia nchini Tanzania Profesa RATLAN PARDEDE yenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya mkoa wa SIMIYU na nchi ya Indonesia.

Pardede amesema Indonesia itashirikiana na mkoa wa SIMIYU kwenye sekta ya viwanda vya pamba na ngozi ili kuongeza thamani ya mazao hayo huku akiahidi kuwaalika wafanyabiashara wa Indonesia katika sekta ya viwanda vya nguo kuja kuanzisha viwanda hivyo mkoani SIMIYU .

Akimkaribisha balozi huyo wilayani MASWA  mkuu wa mkoa wa SIMIYU  ANTHONY MTAKA amesema ujio wa balozi huyo unalenga kuongeza na kukuza wigo na fursa za kibiashara baina ya SIMIYU na nchi hiyo huku akieleza namna upanuaji wa kiwanda cha chaki cha MASWA utakavyosaidia kuondoa ushuru na tozo kwa wafanyabiashara wadogo .

Awali akiongea baada ya balozi kutembelea kiwanda cha chaki, mkuu wa wilaya ya MASWA SEIF SHEKALAGHE  amewataka vijana kujiunga kwenye vikundi ili kukuza uchumi wa viwanda sambamba na kushirikiana na serikali ili kujiletea maendeleo.

Kwa upande wake meneja wa kiwanda cha kuchambua pamba cha ALLIANCE  GINNERY  BOAZ OGOLA amesema kuwa ujio wa balozi umefungua milango huku akiahidi kutoa ushirikiano.

Balozi RATLAN PARDEDE anafanya ziara ya siku nne mkoani Simiyu kufuatia mwaliko wa mkuu wa mkoa huo ili kukuza ushirikiano wa kibiashara kati ya Indonesia na mkoa wa Simiyu.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>