Published On: Sat, May 19th, 2018

Harusi ya Kifalme ya Prince Harry na Meghan Markle: Mwanamfalme Harry na Meghan wafunganishwa katika ndoa Windsor Castle

Share This
Tags

Bi Meghan Markle na Mwanamfalme Harry wamevishana pete na kutangazwa kuwa mume na mke Windsor Castle katika sherehe inayofuatiliwa na mamilioni ya watu kupitia runinga, mtandao na redio.

Wawili hao walifungishwa ndoa mbele ya Malkia na wageni 600 waliokuwemo ndani ya kanisa la St George, katika Windsor Castle.

Bi Markle alikuwa amevalia vazi la harusi lililoshonwa na fundi mbunifu wa mitindo Mwingereza Clare Waight Keller.

Bi Meghan alitumia gari aina ya Rolls Royce Phantom kufika kanisani ambapo alipokelewa kwa shangwe na nderemo aliposhuka kutoka kwenye gari hilo na kuingia kanisa la St George.

Miongoni mwa wageni waliofika ni nyota wa televisheni Marekani Oprah Winfrey na mwigizaji Idris Elba.

George na Amal Clooney, David na Victoria Beckham pamoja na Elton John pia wamewasili.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>