Published On: Wed, May 2nd, 2018
Sports | Post by jerome

Gor Mahia yaifunga AFC Leopards na sasa itacheza na Hull City Mei 13

Share This
Tags

Klabu ya Gor Mahia jana imepata ushindi wa 5-4 kwa njia ya penati, dhidi ya mahasimu wao wa kihistoria kwenye soka la Kenya AFC Leopards kwenye mechi ya kuwania nafasi ya kucheza na Hull City ya Uingereza mnamo Mei 13 mjini Nairobi.

Katika mchezo huo wa jana uliopigwa mjini Nakuru, timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana katika dakika 90 ndipo moja kwa moja wakaenda hatua ya penati.

Hii itakuwa timu ya pili kutoka Uingereza kucheza na Gor Mahia kwani mwezi Julai mwaka jana ilicheza na Everton baada ya kushinda taji la SportPesa la Afrika Mashariki.

Mechi hiyo ilihudhuriwa na waziri mkuu wa zamani wa nchi Raila Odinga, na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Sportpesa ambao ndiyo wadhamini wakuu wa Gor Mahia, AFC Leopards na Hull City ya Uingereza.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>