Published On: Tue, May 8th, 2018

Filamu iliyopigwa marufuku Kenya kuonyeshwa katika tamasha la filamu Cannes

Share This
Tags

Tamasha la kimataifa la Cannes linaanza hii leo, siku moja mapema kama ilivyokawaida, na sheria mpya pia zimebuniwa kuhakikisha kila kitu kinaendela shwari kama kawaida.

Wageni wanaojipiga picha za ‘selfy’ kwenye zulia jekundu wanazuiliwa kama njia ya kukomesha tamaduni hiyo iliyokuwepo hapo awali.

Upeperushaji wa tamasha hilo kwa mara ya kwanza na vyombo vya habari kwa ulimwengu mzima hautafanyika tena kama ilivyokuwa awali.

Tamasha hiyo itashirikiana na serikali ya Ufaransa kubuni nambari za usaidizi kwa wanawake kuweza kuripoti visa vya unyanyasaji wa kingono.

Hii ni baada ya madai ya mzalishaji wa filamu Harvey Weinstein kumbaka muigizaji na kukosa maadili mema wakati wote anapohudhuria tamasha hizo.

Weinstein amepinga madai yote ya kufanya mapenzi bila idhini.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>