Published On: Tue, May 15th, 2018

Dawa ya kutibu mafua inatafitiwa

Share This
Tags

Tiba ya Mafua ya kawaida huenda ikapatikana . Wanasayansi katika chuo cha Imperial College London waanarifu kuwa tiba yake itahusisha uzuiaji wa protini muhimu katika seli za mapafu ambazo virusi vya mafua kwa kawaida hushambulia , kuzaliana na kusambaa .

Watafiti wa magonjwa mbalimbali wanasema kwamba dawa hiyo inaoneka haina madhara kwa kwa seli za binadamu na inaweza kusidhibitiwa kwa kupitia kifaa kidogo kinachobebeka kwa urahisi na dawa kupitishiwa puani.

Watafiti hao wametoa muda maalumu wa majaribio ya kibinadamu kwamba yanaweza kuanza ndani ya miaka miwili.

Mafua yanaenea kwa urahisi sana kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mtu mwingine.Na virusi vya ugonjwa huo ambavyo husababisha uambukizo vianuwezo wa kuishi kwenye mikono na hata na nyuso kwa saa 24.

Dawa za kuzuia maumivu na tiba baridi inaweza kusaidia kupunguza dalili. Lakini kwa sasa hakuna kitu ambacho kitazuia maambukizo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>