Published On: Wed, May 16th, 2018
World | Post by jerome

Daktari ashtakiwa kuiba moyo wa marehemu Kenya

Share This
Tags

Mkuu wa zamani wa uchunguzi wa chanzo cha vifo Kenya ameshtakiwa kosa la kuiba moyo kutoka kwenye maiti iliyokuwa inafanyiwa upasuaji.

Dkt Moses Njue alikanusha shtaka hilo aliposomewa mashtaka katika mahakama ya Hakimu Mkuu Nairobi.

Dkt Njue alikuwa ameshtakiwa kwamba yeye, pamoja na mwanawe, Lemuel Anasha Mureithi, ambaye hakuwepo kortini na ambaye alikuwa mchunguzi msaidizi wake.

Walidaiwa kuiba moyo wa Timothy Mwandi Muumbo wakifanyia mwili wake upasuaji 25 Juni, 2015 katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Lee Funeral Home.

Hakimu Mkuu Francis Andayi aliagiza Bw Mureithi afike mahakamani na kujibu mashtaka kabla ya kesi kuanza kusikizwa 3 Julai.

Dkt Njue alikanusha pia shtaka jingine la kuuharibu moyo ili kuficha ushahidi , akifahamu kwamba ripoti ya uchunguzi wa maiti hiyo ingetumiwa kwenye kesi iliyokuwepo kortini.

Alishtakiwa pia kosa la tatu la kuuondoa moyo huo kutoka kwenye maiti bila idhini, kosa ambalo pia alilikanusha.

Mahakama ilikuwa awali imekataa ombi la Dkt Njue la kuahirisha kusomewa kwa mashtaka akisema jamaa zake Muumbo walikuwa wamewasilisha kesi jingine Mahakama ya Kuu kumtaka kuutoa moyo huo.

Dkt Njue alikuwa amesema kesi hiyo itaingilia kesi hiyo iliyo Mahakama Kuu.

Lakini Hakimu Andayi alikubaliana na upande wa mashtaka na kusema hakuna msingi wowote wa kuzuia kesi hiyo iliyokuwa mbele yake kuendelea.

Dkt Njue aliachiliwa kwa dhamana ya Sh300,000 (dola 3,000 za Marekani) pesa taslimu.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>