Published On: Wed, May 9th, 2018
Business | Post by jerome

Bei ya gesi kwa maskini yapunguzwa Kenya

Share This
Tags

Wizara ya fedha nchini Kenya imetoa shilingi bilioni 2 za kusaidia kupunguzwa bei ya gesi kwa familia masikini.

Sasa mtungi mmoja wa gesi wa kilo sita utauzwa kwa shilingi 2,000 badala ya elfu 5,000.

Kutolewa kwa fedha hizo ni mpango wa serikali wa kupunguza utegemeaji wa mkaa na mafuta taa kwa shughuli za upishi.

Mitungi ya gesi kwa jina Gas Yetu, itasambazwa kwa familia maskini kupitia kampuni ya kuuza mafuta ya National Oil.

Chini ya mpango huo ambao umefanyiwa majaribio katika kaunti za Machakos na Kajiado wizara ya kawi inapanga kununua na kusambaza mitungi milioni 1 ya gesi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>