Published On: Tue, May 15th, 2018
World | Post by jerome

Akina mama waandamana kwa hasira kushinikiza haki ya mama kumyonyesha mwana Kenya

Share This
Tags

Wanawake walio na hasira wameandamana leo mjini Nairobi kulalamika tuhuma za kufukuzwa kwa mwanamke mmoja kutoka mgahawa mmoja kwa kumyonyesha mtoto wake.

Wanawake hao wameelekea katika mgahawa wa Olive Restaurant, ambako mama huyo anatuhumu kuwa aliambiwa ajifunike wakati anamnyonyesha mtoto wake mwenye mri wa mwaka mmoja.

Alieleza kisa kilichompata katika kundi moja la akina mama katika mtandao wa kijamii Facebook, na kusema kuwa aliambiwa akamyonyeshe mtoto wake chooni, jambo lililomuacha akihisi kudharauliwa.

Taarifa hiyo imezusha hisia kali kote nchini na kusababisha makundi ya kutetea haki za wanawake kuandaa maandamano ya leo mjini.

Mgahawa huo umeomba utulivu udumishwe kufutia ghadhabu hiyo kubwa ya wanawake nchini ukiomba kupewa muda kulishughulikia suala hilo kwa ndani.

Mojawapo ya mashirika yalioshiriki maandamano hayo leo ni Muungano wa mawakili wanawake FIDA.

Unasema dhamira kuu ya maandamano ya leo ni kushinikiza haki za akina mama waungwe mkono na kusaidiwa katika kufanikisha kuwanyonyesha watoto wao bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>