Published On: Tue, Apr 10th, 2018
World | Post by jerome

Zuckerback ajitwika lawaka kutokana matumizi mabaya ya data

Share This
Tags

Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Facebook Mark Zuckerberg amekiri kuwa mtandao huo wa kijamii haujafanya vya kutosha kuzuia matumizi mabaya ya data za watumiaji wake, na kujitwika lawama zote.

Kauli ya mkuu huyo wa Facebook mwenye umri wa miaka 33, imetolewa kabla ya kufika mbele ya kamati za bunge la Marekani hii leo na kesho Jumatano. Kampuni hiyo inakabiliwa na mgogoro mbaya zaidi unaohusu usiri katika historia yake ya miaka 14 baada ya wafichuzi wa siri kusema kuwa maelezo binafsi ya mamilioni ya watumiaji wake, hasa nchini Marekani, yalitolewa kwa kampuni ya huduma za ushauri wa kisiasa ya Cambridge Analytica.

Kampuni hiyo ya Cambridge Analytica yenye makao yake jijini London, ambayo inajumuisha kampeni ya uchaguzi wa Rais wa Marekani Donald Trump kuwa miongoni mwa wateja wake wa nyuma, inapinga idadi hiyo iliyotolewa ya watumiaji walioathirika.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>