Published On: Mon, Apr 16th, 2018

WAZEE MWANZA: TUNAOMBA TUJENGEWE UZIO

Share This
Tags

Wazee wanaoishi katika kituo cha makao ya wazee cha Bukumbi kilichopo wilayani Misungwi mkoani Mwanza wameiomba serikali kuwajengea uzio katika kambi hiyo  kwa kuhofia vitendo vya mauaji na ukataji wa viungo vya mwili hasa sehemu za siri za wanawake vilivyojitokeza katika wilaya hiyo.

Kambi hii maalumu imewakusanya wazee wasiojiweza kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo wenye ulemavu ambao huhudumiwa na serikali.

Mamlaka ya usimamizi wa bandari mkoani Mwanza kwa kuwakumbuka wazee hao imetembelea kambi hiyo ya wazee ya  Bukumbi na kupeleka msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo chakula.

 

 

DORMANA PIMA ni mlezi msaidizi wa makao ya wazee wasiojiweza Bukumbi na HELEN EMMANUEL ni mwenyekiti wa kambi hiyo ambaye ameshukuru kwa msaada huo wa chakula.

Mamlaka ya usimamizi wa Bandari mkoani Mwanza imepeleka msaada wa mchele, unga, mafuta ya kupikia, sukari pamoja na sabuni.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>